Kutoka katika ripoti ya Forbes, Jolie katika kipindi cha mwezi June mwaka jana na June mwaka huu, ameingiza kiasi cha dola milioni 33 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 48 za kitanzania.
Forbes imesema mrembo huyo amekusanya mkwanja kutokana na deal ya kushiriki katika filamu mpya ya Maleficent aliyolipwa dola miloni 15 na inatarajiwa kutoka mwakani.
Pia ameingiza dola milioni 10 akiwa kama balozi wa brand maarufu, Louis Vuitton.
Jennifer Lawrence amechukua nafasi ya pili kutoka na kuvuna mkwanja wa dola milioni 26 alizoingiza kupitia filamu zake Hunger Games na Playbook Silver Linings
Kristen Stewart amekamata nafasi ya tatu kwa kuvuna mkwanja wa dola milioni 22. Mwaka jana alikuwa mwigizaji anayelipwa zaidi.
Jennifer Aniston amekamata nafasi ya nne kwa kuingiza dola milioni 20.
Nafasi ya tano imekamatwa na Emma Stone aliyeingiza dola milioni 16.
Alicheza katika filamu ya bajati kubwa “The Amazing Spider-Man”.
Charlize Theron amekamata nafasi ya sita kwa kuvuna dola milioni 15.
Nafasi ya saba ni Sandra Bullock aliyevuna mkwanja wa dola milioni 14.
Natalie Portman ni mshindi wa Oscar katika filamu ya No Stranger to Big Blockbuster amevuna mkwanja wa dola milioni 14 na kukamata nafasi ya nane.
9 Mila Kunis dola milioni 11
10.
Julia Roberts dola milioni 11
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment