Papa Francis Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani amekiri kushindwa
kupambana na vitendo vya ufisadi na lobi ya watu wanaopenda kufanya
ngono ya jinsia moja vilivyoshamiri huko Vatican.
Akizungumza na wajumbe
wa Mashirikisho ya Kidini ya Amerika ya Latini, Papa Francis
amesisitiza kuwa, ndani ya Vatican kuna ufisadi mkubwa pamoja na lobi ya
watu wanaofanya ngono ya jinsia moja.
Ameongeza kuwa, kwa miongo kadhaa
sasa Kanisa Katoliki limekumbwa na migogoro mikubwa ya ufisadi ,
utumiwaji mbaya wa mali za kanisa, kuporomoka maadili na hasa suala la
ubakaji watoto wanaopata mafunzo kwenye makanisa ya madhehebu hiyo
katika nchi mbalimbali na hasa Marekani na Ulaya.
Papa Francis amekiri
kushindwa kuupatia ufumbuzi mgogoro huo, na hivyo ameamua kulikabidhi
kwa kamati ya makadinali wenye kuaminika, ili waweze kulishughulikia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment