Main Menu

Thursday, June 13, 2013

WAANDISHI WA HABARI ZA UHIFADHI NA UTALII WA NDANI WAPEWA TUZO MKOANI IRINGA.


Pichani nyuma ni Washindi wa tuzo mbalimbali kupitia Televisheni, Redio na Magazeti wakiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya Meza kuu.
Waziri wa Maliasili na utalii Balozi Khamis Kagasheki akimkabidhi Mwandishi David Azaria wa Sahara Media Group,mfano wa hundi ya shilingi milioni moja na laki tano aliyoshinda baada ya kuandika makala nzuri ya kutangaza utalii wa Tanzania katika tuzo ilioyoandaliwa na shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA) kwa waandishi wa habari wa Televisheni, Redio na Magazeti katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa tuzo hizo iliyofanyika kwenye hoteli ya Hilltop Hotel ya mjini Iringa.

Hafla hiyo imefanyika baada ya mkutano wa siku mbili kati ya TANAPA na Wahariri wa vyombo vya habari,kauli mbiu ilihusu juu ya Jukumu la Vyombo vya habari Katika kukabiliana na Ujangili katika hifadhi za taifa, kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Ndugu James Lembeli na katikati ni Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi. 

Tuzo hizo zililenga kuhamasisha vyombo vya habari kuandika makala,habari kuandaa vipindi vya redio na televisheni,vinavyolenga kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kuenzi uhifadhi kwa faida ya kizazi hiki na kijacho.

Vyombo vya habari vinapaswa kuelimisha umma juu ya umuhimu wa kuhifadhi maeneo ya hifadhi kwa kukemea wavamizi wa maeneo ya hifadhi ama kwa kulisha mifugo,kukekemea uzibwaji wa maeneo ya mapito ya wanyama na changamoto nyinginezo.

Aidha katika tuzo hizo,Mshindi wa kwanza alizawadiwa kiasi shilingi milioni moja na laki tano,cheti,ngao pamoja na safari ya siku katika mojawapo ya nchi za kusini mwa Afrika kwa ajili ya kutembelea maeneo ya hifadhi na vyombo vya habari vinavyohusika na utalii wa ndani,mshindi wa pili Cheti na fedha kiasi cha shilingi milioni moja na mshindi wa tatu alipewa kiasi cha shilingi laki tano pamoja na cheti.
Waziri wa Maliasili na utalii Balozi Khamis Kagasheki akimkabidhi Mwandishi Alex Magwiza wa TBC tuzo aliyojishindia baada ya kuandika makala iliyozungumzia vyema masuala ya utalii wa ndani, kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Ndugu James Lembeli na katikati ni Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi.
Waziri wa Maliasili na utalii Balozi Khamis Kagasheki akimkabidhi mfano wa hundi na ngao Mwandishi Festo Sikagonamo wa ITV ,mara baada ya kushinda kutangaza vyema makala iliyozungumzia masuala ya uhifadhi wa mbuga zetu za Taifa, kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Ndugu James Lembeli na katikati ni Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi.
Waziri wa Maliasili na utalii Balozi Khamis Kagasheki akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni moja na laki tano Mwandishi wa gazeti la Nispashe,Salome Kitomari kwa kuandika kwa ufasaha makala iliyozungumzia vyema masuala ya utalii wa ndani, kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Ndugu James Lembeli na katikati ni Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi.
Waziri wa Maliasili na utalii Balozi Khamis Kagasheki akimkabidhi Mwandishi David Rwenyagila wa Radio 5 ya Arusha, tuzo aliyojishindia baada ya kuandika makala iliyozungumzia vyema masuala ya uhifadhi wa mbuga zetu za Taifa, kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Ndugu James Lembeli na katikati ni Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi.
Waziri wa Maliasili na utalii Balozi Khamis Kagasheki akimkabidhi Mtangazaji wa televisheni Antonio Nugas wa Clouds Media Group tuzo aliyojishindia baada ya kutangaza vyema masuala ya utalii wa ndani, kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Ndugu James Lembeli na katikati ni Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi. 
Waziri wa Maliasili na utalii Balozi Khamis Kagasheki akimkabidhi Mwandishi Lilian Shirima wa TBC tuzo aliyojishindia baada ya kuandika makala iliyozungumzia vyema masuala ya utalii , kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Ndugu James Lembeli na katikati ni Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi. 
Waziri wa Maliasili na utalii Balozi Khamis Kagasheki akimkabidhi Mwandishi Albano Midelo wa Gazeti la Dira,mfano wa hundi ya shilingi milioni moja na laki tano,aliyojishindia baada ya kuandika makala iliyozungumzia vyema masuala ya hifadhi ya Taifa,kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Ndugu James Lembeli na katikati ni Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi.

0 comments:

Post a Comment