Dirisha la usajili linategemewa kufunguliwa hivi karibuni
na zipo taarifa nyingi kuhusiana na masuala ya usajili.
Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Manchster United zimesema
kuwa klabu hiyo imekubaliana na beki wa kati wa klabu ya Valencia na timu ya
taifa ya Argentina Nicolas Otamendi.
Kwa mujibu wa jarida la Diario Ole la Argentina,Otamendi
amekwishakubaliana maslahi yake binafsi na klabu ya Manchster United na
kinachosubiriwa ni kwa mchezaji huyo kumaliza michuano ya Copa America ili
ajiunge na mashetani hao wekundu.
0 comments:
Post a Comment