Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kufanyika kwa
uchaguzi wa Shirikisho la soka Duniani FIFA, mmoja kati ya wagombea wa kiti cha
Urais Michael Van Praag ambaye pia ni Rais wa chama cha soka nchini Uholanzi
amejiondoa kugombea nafasi ya Urais.
Michael Van Praag kwa sasa ana umri wa miaka 67 na alikuwa
miongoni mwa wagombea watatu ambao walikuwa wakiwania kiti cha Urais wa
Shirikisho la soka duniani FIFA.
Wengine ni pamoja na Prince ali Bin Ali Hussein na
mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Ureno Luis Figo.
Minong’ono na tetesi za kuwa Michael hatagombea kiti cha
Urais zilianza hapo jana.
Kujiondoa kwa Michael Van Praaga kunamaanisha kuwa nafasi
ya wagombea wa Urais wa kiti hicho watabakia watatu ambao ni Joseph Sepp
Blatter,Princ Ali Bin Hussein na Luis Figo.
Uchaguzi wa FIFA unatarajiwa kufanyika mnamo tarehe 29 ya
mwezi huu wa tano mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment