Kiungo wa klabu ya Arsenal Santi Cazorla hapo jana
aliweka rekodi ya kuwa mpiga pasi bora katika Ligi Kuu ya soka nchini England
na kumpita kiungo wa Chelsea Cesc Fabregas katika mchezo kati ya Arsenal dhidi
ya Sunderland.
Rekodi ya Cazorla inahusisha upigaji wa pasi sahihi na
zilizofika katika mchezo mmoja.
Rekodi ya Cazorla hapo jana katika mchezo wa Arsenal
dhidi ya Sunderland ni kupiga jumla ya pasi 155 ndani ya dakika 90.
Rekodi hii inavunja ile rekodi ya Fabregas ya kupiga pasi
144 ndani ya dakika 90 katika mchezo kati ya Chelsea na West Bromwich Albion.
Match
|
Accurate Pass
|
Mins
Played
|
|
Santiago
Cazorla
|
Arsenal vs Sunderland
|
155
|
90
|
Cesc
Fàbregas
|
Chelsea vs West Brom
|
144
|
90
|
Cesc
Fàbregas
|
Chelsea vs Aston Villa
|
133
|
90
|
Yaya
Touré
|
Aston Villa vs Man City
|
128
|
90
|
Fernandinho
|
Sunderland vs Man City
|
126
|
90
|
Cazorla hakuishia hapo kwani aliweka rekodi nyingine ya
kuwa mchezaji aliyegusa mpira mara nyingi kuliko mchezaji mwingine yoyote ndani
ya dakika 90 za mchezo mmoja.
Cazorla aligusa mpira mara 178 dhidi ya Sunderland na
kumpita Fabregas aliyewahi kugusa mpira mara 174 katika mchezo wa Chelsea dhidi
ya West Bromwich Albion.
Match
|
Touches
|
Mins
Played
|
|
Santiago
Cazorla
|
Arsenal vs Sunderland
|
178
|
90
|
Cesc
Fàbregas
|
Chelsea vs West Brom
|
174
|
90
|
Cesc
Fàbregas
|
Chelsea vs Aston Villa
|
162
|
90
|
Aaron
Ramsey
|
Arsenal vs Sunderland
|
156
|
90
|
Rekodi ya mwisho ya Cazorla ni ya kupiga pasi nyingi
katika theluthi ya mwisho ya timu pinzani.
Cazorla alipiga jumla ya pasi 86 ndani ya dakika 90 katika
mchezo dhidi ya Sunderland, Cazorla anavunja rekodi ya David Silva aliyefanikiwa
kupiga pasi 82 ndani ya dakika 90 katika eneo la mwisho la West Bromwich Albion
katika mchezo kati ya Manchester City dhidi ya West Bromwich Albion.
Match
|
Successful
Final Third Passes
|
Mins
Played
|
|
Santiago
Cazorla
|
Arsenal vs Sunderland
|
86
|
90
|
David
Silva
|
Man City vs West Brom
|
82
|
81
|
Aaron
Ramsey
|
Arsenal vs Sunderland
|
68
|
90
|
Cesc
Fàbregas
|
Chelsea vs West Brom
|
64
|
90
|
Mesut
Özil
|
Arsenal vs Swansea
|
64
|
90
|
0 comments:
Post a Comment