Mchezaji wa timu ya mpira wa kikapu ya San Antonio Spurs
Kawhi Leonard amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ulinzi wa Ligi ya mpira wa
kikapu nchini Marekani ‘NBA’.
Tuzo hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya magari ya Kia imemshuhudia
Kawhi akiwashinda nyota wengine kama Draymond Green, Tony Allen na Deandre
Jordan.
Katika kura za awali Draymond Green wa Timu ya Golden
State Warriors alionekana kumshinda Kawhi Leonard lakini kadiri kura
zilivyokuwa zikiendela kupigwa, Kawhi aliweza kupata jumla ya kura 242 huku
mpinzani wake Draymond Green akipata kura 229 tu.
Tuzo za mchezaji bora wa Ulinzi katika NBA hutolewa na
chama cha waandishi wa Habari za mpira wa kikapu nchini Marekani kwa kuwapigia
kura wachezaji waliopendekezwa katika idara hiyo ya ulinzi.
Utoaji wa tuzo hiyo uliambatana na upangwaji wa vikosi
viwili vya idara ya ulinzi.
Kikosi cha kwanza kilikuwa na nyota waliopata alama za
juu katika upigaji kura wa mlinzi bora na kikosi cha pili kilihusisha wachezaji
walioshika nafasi nyingine kwa mujibu wa kura za waandishi.
Kikosi cha kwanza kinamjumuisho wa mshindi wa tuzo ya
mchezaji bora wa ulinzi Kahi Leonard
toka San Antonio Spurs, Deandre Jordan( LA Clippers),Tony Allen (Memphis),Chris
Paul ( LA Clppers) na Draymond Green (Golden State Warriors).
Kikosi cha pili kina nyota kama Anthony Davis (New Orleans Pelicans),Jimmy Butler (Chicago
Bulls),Andrew Bogut (Golden State Warriors),John Wall (Washington Wizards) n a
Tim Duncan ( San Antonio Spurs).
0 comments:
Post a Comment