Kamati
ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF inatarajiwa
kukutana jumapili tarehe 24, Mei mwaka huu ikiwa ni kikao cha kawaida
cha kamati hiyo.
Moja
ya ajenda katika kikao hicho itakua ni kupokea na kujadili mienendo,
maandalizi na maendeleo ya timu za Taifa za mpira wa miguu nchini.
Pamoja na kuwa kikao hicho ni chakawaida lakini kitakua kimesukumwa zaidi na mwenendo usiopendeza wa timu ya taifa katika mashindano ya COSAFA yanayoendelea nchini Afrika ya kusini.
0 comments:
Post a Comment