Main Menu

Thursday, April 4, 2013

WABUNGE NCHINI KENYA WATAKA KUONGEZEWA MSHAHARA

                             jengo la bunge la kenya

Wabunge waliochaguliwa hivi karibuni nchini Kenya wanataka kuongezewa mshahara wao hata kabla ya vikao rasmi vya bunge kuanza.

Wabunge hao ambao mishahara yao ilipunguzwa kwa asilimia 37 na kufika karibu laki tano wamelalamika na kusema mshahara huo ni mdogo sana.

Tume ya Huduma ya Bunge PSC imesema inashauriana na Tume ya Mishahara Kenya SRC kwa lengo la kutafuta suluhisho kufuatia malalamiko ya wabunge.

Tume hiyo ya mishahara ilipunguza mishahara ya wabunge kutoka Shilingi 851,000 hadi 532,400 jambo ambalo limewakasirisha wabunge wapya. 

Tume hiyo inasema hatua ya kupunguza mishahara ya wabunge ni katika fremu ya kubungza bajeti kubwa ya mishahara ya maafisa wa ngazi za juu nchini Kenya.

Hivi karibuni Rais-mteule wa Kenya Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto walionya kuwa Kenya haiwezi kumudu gharama za mishahara na hivyo wamesema serikali yamkini ikapunguza mishahara hiyo au kusimamisha nyongeza ya mishahara. 

Wawili hao wamesema huenda Kenya ikapoteza nafasi yake ya kiuchumi barani Afrika kutokana na bajeti kubwa ya mishahara.

0 comments:

Post a Comment