Main Menu

Thursday, June 13, 2013

HALI YA MANDELA YAELEZWA KUENDELEA VYEMA

     Nelson Mandela akiwa amebeba kombe la Dunia mwaka 2010

Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma amesema kuwa Rais mstaafu Nelson Mandela anaendelea vyema na matibabu baada ya kile alichokitaja kuwa siku chache ngumu.

Mandela amelazwa hospitalini mjini Pretoria tangu siku ya Jumamosi iliyopita, akiugua maradhi ya mapafu hii ikiwa ni mara ya nne, kwa kiongozi huyo kulazwa hospitalini tangu mwezi Desemba mwaka jana.

Mandela mwenye umri wa miaka 94, alifungwa gerezani kwa miaka 27 baada ya kushitakiwa kwa kosa la kufanya njama ya kuipindua serikali iliyoongozwa na wazungu walio wachache nchini humo.

Baada ya kutoka jela alihudumu kama Rais wa kwanza wa Afrika kusini mweusi kuanzia mwaka 1994 hadi mwaka 1999. 

0 comments:

Post a Comment