Mwanasoka mahiri Lionel Messe anatuhumiwa
kwa kukwepa kulipa kodi.
Messi pamoja na baba yake
wanashutumiwa na waendesha mashitaka mjini Catalonia nchini
Uhispania kwa kukwepa kulipa kodi kwa ofisi ya kodi katika eneo
hilo ya kiasi ya euro milioni 4 kati ya mwaka 2007 na 2009 kutokana
na mapato ya ziada mchezaji huyo alipokea kutokana na kushiriki
katika kuonekana katika mauzo ya kibiashara.
Messi mwenye umri
wa miaka 25 ndiye mwanasoka aliyeifungia Barcelona mabao mengi
zaidi katika historia ya kilabu hiyo na ameshinda tuzo ya mchezaji
bora wa shirikisho la soka duniani Fifa kwa miaka minne mfululizo.
Thursday, June 13, 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment