Mchuuzi mmoja wa sigara nchini Tunisia amejiwasha moto hii leo katika mji
mkuu Tunis saa chache kabla ya wabunge wa nchi hiyo kuingia katika
mchakato wa kuipigia kura serikali mpya inayotegemewa kuiondoa nchi hiyo
kutoka katika mgogoro wa kisiasa.
Adel Khadri mwenye umri wa miaka 27
amepata majeraha mabaya kutoka na moto huo .
Inadaiwa kwamba kijana
huyo anatokea katika familia masikini kabisa katika eneo la Jendouba
Kaskazini magharibi ya Tunisa na alikwenda katika mji mkuu huo wa Tunis
miezi michache iliyopita kwa ajili ya kutafuta ajira.
Tukio hilo la kujiwasha moto
limetokea katika eneo ambako ni kitovu cha vuguvugu la mwaka 2011
lililosababisha kuondolewa madarakani aliyekuwa dikteta wa nchi hiyo Zine El
Abidine Ben Ali.
0 comments:
Post a Comment