Macho na masikio ya Wakatoliki yameelekezwa Vatican, ambapo makardinali 115 wameanza kikao cha kumchagua Papa mpya.
Mkutano wa makardinali unafanyika kwa faragha katika kanisa la Sistine na hautamalizika mpaka Papa mpya atakapopatikana.
Hakuna anayesema ni muda gani utachukua.
Hata hivyo, punde utakapoonekana moshi mweupe ukitoka kwenye dohani, itakuwa dhahiri kwamba kanisa Katoliki limepata kiongozi mpya.
Atakayechaguliwa lazima apate kura 77 ambazo ni sawa na theluthi mbili ya wapiga kura wote.
Hii ni mara ya kwanza tangu baada ya miaka 600 kwa Makadinali kufanya kikao kama hicho wakati Papa wa zamani bado yuko hai.
Hii ni kufuatia hatua ya Papa Benedict wa XIV kujiuzulu wadhifa wake Februari 28 kwa madai ya kudorora kwa afya yake.
0 comments:
Post a Comment