Mapigano na purukushani zilizotokea kati ya wafuasi wa mwanamke mmoja
anayedai kuwa mtaalamu wa elimu ya kiroho nchini Burundi, zimepelekea
watu wasiopungua sita kuuawa.
Tukio hilo limetokea mapema leo baada ya
polisi wa Burundi kukabiliana na wafuasi wa Bi Zebiya ambaye anadai
kujiwa na Bibi Maryam (AS) mama wa Yesu yaani Nabii Isa AS, ambapo watu
sita wameuawa na wengine 35 kujeruhiwa katika tukio hilo.
Mapigano hayo
yalitokea asubuhi na mapema wakati mamia ya wafuasi wa Bi Zebiya mwenye
umri wa miaka 30 walipokuwa wamekusanyika juu ya mlima mmoja nchi humo.
P
olisi ya Burundi imesema kuwa, polisi wanne walijeruhiwa vibaya katika
mapigano hayo.
Bi Zebiya anadai kuwa, tarehe 12 ya kila mwezi ana uwezo
wa kumuona Bibi Maryamu (AS) katika mlima ambao sasa umegeuka kuwa
pahala patakatifu kwa wafuasi wake.
radio tehran
0 comments:
Post a Comment