Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars)
ambayo inadhaminiwa na kampuni ya bia ya Kilimanjaro, leo inaingia kambini
katika hoteli ya Tansoma iliyopo eneo la Gerezani kujiandaa na mchezo dhidi ya
Misri kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika (AFCON).
Kikosi kitakachoingia kambini
kinawajumuisha wachezaji waliocheza michuano ya Cosafa nchini Afrika Kusini
mwishoni mwa mwezi Mei, wachezaji 20 walioanza kambi tangu wiki iliyopita na
wachezaji wanaocheza soka la kulipwa nchini Congo DR.
Taifa Stars inatarajiwa kufanya mazoezi
katika uwanja wa Gymkana na Uwanja wa Taifa kwa muda siku mbili kabla ya siku
ya alhamis kusafiiri kuelekea Addis Ababa nchini Ethiopia ambapo itaweka kambi
ya wiki moja kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri.
Wachezaji wanaotarajiwa kuingia kambini leo
ni Deogratias Munish, Mwadini Ali, Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Haji Mwinyi,
Aggrey Morris, Salum Mbonde, Erasto Nyoni, Saimon Msuva, Hassan Dilunga, Joram
Mgeveke, Juma Liuzio, Said Ndemla, Mwinyi Kazimoto, Abdi Banda, John Bocco,
Mrisho Ngasa, Salum Abubakar, Ibrahim Ajibu, Thomas Ulimwengu na Mbwana
Samatta.
Wachezaji waliopo kambini tangu wiki
iliyopita ni Nadir Haroub, Juma Abdul, Salum Telela, Peter Manyika jr, Jonas
Mkude, Hassan Isihaka, Mohamed Hussein, Aishi Manula, Frank Domayo, Mudathir
Yahya, Kelvin Friday, Malimi Busungu, Bennedict Tinoco, Rashid Mandawa, Atupele
Green, Haroun Chanongo, Emmanuel Simwanda, Said Mohamed, Andrew Vicent, Gadiel
Michael, Deus Kaseke.
Msafara wa Taifa Stars unatarajiwa kuondoka
nchini Alhamis Juni 4, 2015 kuelekea Ethiopia ukiwa na wachezaji 23,benchi la
ufundi pamoja na viongozi .
Mechi kati ya Misri dhidi ya Tanzania
inatarajiwa kuchezwa Juni 14, 2015 katika uwanja wa Borg El Arab pembeni
kidogo ya jiji la Alexandria.
0 comments:
Post a Comment