Meja mstaafu Abdul Mingange aliyesimama.
Timu ya ndanda fc ya mkoni mtwara imetangaza kuachana na kocha wake Meja mstaafu Abdul Omary Mingange baada ya kuiongoza timu hiyo robo tatu ya msimu na kufanikiwa kuibakisha ligi kuu.
Meja mingange alijiunga na Ndanda Fc akichukua mikoba ya Denis Kitambi aliyeiongoza timu hiyo mwanzoni mwa msimu baada ya kuipandisha ligi kuu.
Msemaji wa timu hiyo Idrisa Bandari ameuambia mtandao huu kuwa wanamshukuru na wanathamini mchango wake kwenye timu hiyo hasa kuibakisha ligi kuu.
Bandari amesema baada ya kuachana na mingange wamempa mkataba wa mwaka mmoja kocha Jumanne Charles kwa ajili ya msimu ujao.
Hata hivyo kocha msaidizi ataendelea kuwa Ngawina Ngawina.
Kabla ya kujiunga na Ndanda fc Jumanne Charles alikua anaifundisha timu ya daraja la kwanza ya Kurugenzi Fc ya wilayani Mufindi mkoani Iringa.
0 comments:
Post a Comment