Timu ya Mbeya City imeendelea kuboresha kikosi chake
baada ya kumsajili mshambuliaji wa timu ya ndanda fc gidion brown.
Kwa mujibu wa website ya timu hiyo Mshambuliaji huyo
ameingia mkataba wa mwaka mmoja na nusu kuwatumikia wagonga nyundo hao wa jiji
la mbeya.
Msimu uliopita Brown alikuwa moja ya wachezaji muhimu
kwenye kikosi cha Ndanda Fc akicheza michezo 21 akiwa kwenye kikosi cha
kwanza, na kuifungia timu hiyo ya Mtwara jumla ya mabao 5.
Awali mshambuliaji huyu amewahi kuchezea timu ya
KMKM ya Zanzibar na kuisaidia kutwaa taji la ligi kuu ya visiwani humo
pia amecheza kwenye kikosi cha Rhino ya Tabora na Moro United.
0 comments:
Post a Comment