Mshambuliaji mpya wa klabu ya Young African Malimi
Busungu ametambulishwa rasmi leo makao makuu ya klabu hiyo.
Katika utambulisho wake Busungu amekabidhiwa jezi namba
16 iliyokua inatumiwa na kiungo Nizah Khalfan anayedaiwa kutimukia timu ya Mwadui
Fc.
Katika utambulisho huo busungu amesema kucheza Young
African ni sehemu ya kukamilika kwa ndoto yake na zaidi ni kuwa timu hiyo
inashiriki michuano ya kimataifa.
Amesema kama ilivyo kwa mchezaji mwingine yoyote ni
vigumu kukataa kuchezea timu kama Young African.
Busungu alisain kuichezea Young Afriican kwa mkataba wa
miaka 2 siku ya jumamosi akitokea timu ya Mgambo JKT aliyoichezea kwa
mafanikio.
Kwa upande wa mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano
wa klabu hiyo Jerry Murro amesema hivi sasa wamefunga usajili wa wachezaji wa
nyumbani na sasa wanaanza usajili wa kimataifa na ikiwezekana wiki ijayo
watamtambulisha moja ya wachezaji bora kabisa afrika.
Kuhusu idadi ya wachezaji ambao wataachwa na timu hiyo
msimu huu, Jerry alikua mgumu kuwataja kwa majina lakini akasisitiza wachezaji
hao tayari wanazo taarifa za kutoendelea kuwa na timu hiyo, na kiashiria cha
kutokua nao ni namba ya jezi walizokua wanavaa kupewa wachezaji wengine.
0 comments:
Post a Comment