Kikosi
cha Kilimanjaro Stars kinaagwa kesho (Novemba 25 mwaka huu) tayari kwa
safari ya Nairobi, Kenya kushiriki michuano ya Kombe la Chalenji
inayoanza kutimua vumbi Novemba 27 mwaka huu.
Hafla
ya kuiaga timu hiyo itafanyika saa 5 asubuhi kambini kwao katika hoteli
ya Accomondia jijini Dar es Salaam. Msafara wa Kilimanjaro Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager utaongozwa na Ahmed Idd
Mgoyi. Timu itaondoka saa 10 alasiri kwa ndege ya RwandAir.
Wachezaji
waliomo katika msafara huo ni makipa Deogratius Munishi (Yanga), Ivo
Mapunda (Gor Mahia, Kenya) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Erasto
Nyoni (Azam), Himid Mao (Azam), Ismail Gambo (Azam), Kelvin Yondani
(Yanga), Michael Pius (Ruvu Shooting) na Said Moradi (Azam).
Viungo
ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga),
Haruna Chanongo (Simba), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Ramadhan
Singano (Simba) na Salum Abubakar (Azam).
Safu
ya ushambuliaji inaundwa na Elias Maguli (Ruvu Shooting), Faridi Musa
(Azam), Joseph Kimwaga (Azam), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Mbwana Samata
(TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngasa (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP
Mazembe, DRC).
Hata
hivyo, washambuliaji Samata na Ulimwengu watajiunga na timu hiyo jijini
Nairobi, Desemba Mosi mwaka huu wakitokea Lubumbashi ambapo Novemba 30
mwaka huu TP Mazembe itacheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Benchi
la Ufundi la timu hiyo linawajumuisha Kim Poulsen (Kocha Mkuu),
Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa Makipa),
Leopold Tasso (Meneja wa Timu), Dk Mwanandi Mwankemwa (Daktari wa Timu),
Frank Mhonda (mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza Vifaa).
Kilimanjaro
Stars ambayo ipo kundi B katika michuano hiyo itacheza mechi yake ya
kwanza Novemba 28 mwaka dhidi ya Zambia kwenye Uwanja wa Machakos.
Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Post a Comment