Usiku wa jana timu
ya Barcelona imetwaa taji la pili msimu huu, baada kuifunga Athletic Bilbao mabao 3-1 katika fainali ya Kombe la Mfalme,
maarufu kama Copa del Rey iliyofanyika katika Uwanja wa Nou Camp.
Lionel
Messi aliendelea kuwa mtu hatari kwa wapinzani wake baada ya kufunga mara mbili huku akionesha uwezo wa hali ya juu pale alipowapangua mabeki wanne wa bilbao na kuifungia Barcelona bao zuri la kwanza
dakika ya 20, kabla ya Mbrazil Neymar kufunga la pili dakika ya 36.
Messi akakamilisha ushindi wa Barca kwa kufunga bao la 3 dakika ya 74, wakati bao la kufutia
machozi la Bilbao lilifungwa na Williams dakika ya 79.
Barca
sasa imechukua mataji mawili kwani awali ilishachukua kombe la La liga sawa na wapinzani wao wa ligi ya mabingwa katika fainal timu ya Juventus ya italia ambao tayari nao wana makombe mawili ya seria A na Copa Italia.
Hivyo kila timu inahitaji ubingwa wa UEFA ili kutwaa makombe matatu.
0 comments:
Post a Comment