Klabu
ya Arsenal jana ilifanikiwa kutetea Kombe la FA baada ya kuichapa mabao 4-0
Aston Villa katika mchezo wa Fainali uliofanyika Uwanja wa Wembley,
London.
Mshambuliaji
Theo Walcott aliifungia bao la kwanza Arsenal kunako dakika ya 40 na Alexis Sanchez akafunga la pili dakika ya 50.
Beki
Mjerumani, Per Mertesacker naye akaifungia bao la tatu timu yake dakika ya 61, kabla ya Olivier Giroud aliyetokea benchi kufunga
la nne dakika ya 90.
Kwa ushindi huo arsenal wamefikisha kombe la 12 la FA na kuizidi Manchester united ambayo imelichukua mara 11.
Huku Wenger akiweka rekodi ya kulichukua taji hilo mara sita ikiwa ni pamoja na Wenger kafanikiwa kulitetea taji hilo.
0 comments:
Post a Comment