Main Menu

Monday, February 10, 2014

MILIONI 25 ZAPATIKANA MCHEZO WA MBEYA CITY DHIDI YA MTIBWA



JUMLA  ya shilingi milioni  25,602,000 zimepatikana katika mechi ya Mbeya City na Mtibwa Sugar iliyochezwa juzi katika uwanja wa kumbukumbu wa Sokoine huku timu  ya Mbeya City ikiondoka na ushindi wa goli 2-1.

Akisoma mapato hayo Katibu  wa chama cha mpira wa miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA) Selemani Harubu , alisema kati mapato hayo shilingi milioni 6,256,097 zimeenda kwa kila timu.

Amesema, gharama ya Vat ni shilingi milioni  3,905,388  tiketi shilingi 489,500 gharama ya mchezo 1,908,639 huku  kamati ya ligi ikiondoka na shilingi 1,908,639.

Amesema,  TFF  imepata shilingi  954,818 na MREFA ikiondoka na shilingi 748,248 na uwanja ukipata shilingi 3,181,056.

Aidha, baadhi ya mashabiki wameuomba uongozi wa MREFA kukaa meza moja ya mazungumzo na   jeshi la polisi mkoa Mbeya  katika kuweka utaratibu mzuri wa kuingia uwanjani tofauti na sasa ambapo inaelezwa kuwa baadhi ya askari wamekuwa ndio chanzo cha vurugu.

Wamesema, mashabiki wamekuwa wakipata usumbufu mkubwa kwa baadhi ya askari polisi ambao hawazingatii  maadili yao ya kazi kwa kuwasumbua watu hata kama hawana kosa lolote.

Hata hivyo katika mchezo huo mbeya city iliibuka kidedea kwa kuichabanga Mtibwa goli 2:1

0 comments:

Post a Comment