POLISI
Mkoani Mbeya, inawashikilia watu wawili kati yao mmoja inasemekana ni askari
wa jeshi la magereza la Ruanda Koplo John Joseph kwa tuhuma za kukutwa na
tiketi bandia za kuingilia uwanjani.
Akizungumzia
sakata hilo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, amesema tukio
hilo limetokea jijini mbeya wakati wa mpambano dhidi ya timu ya
Mbeya City na Mtibwa Sugar katika uwanja wa Sokoine uliopo Jijini Mbeya.
Amesema,
askari polisi wakiwa katika harakati za kuangalia na kulinda hali ya usalama
uwanjani walipata taarifa ya kwamba kuna baadhi ya watu wamekuwa na tiketi
bandia.
Amefafanua
kuwa askari wakishirikiana na Afisa habari wa chama cha mpira wa miguu Mkoa wa
Mbeya(MREFA) Lwitiko Mwandeliwa walifanikiwa kuwatia nguvuni watuhumiwa hao
ambao ni Justin Alphonce(17) na John Joseph ambaye inasemekana ni askari wa
jeshi la magereza na wote ni wakazi wa kota za magereza.
Amesema,
tiketi hizo zilikuwa zikiuzwa kwa shilingi 3000 na kwamba watuhumiwa wote
wapo rumande mpaka upelelezi utakapo kamilika.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa bodi ya michezo katika timu ya Mbeya City, Mussa
Mapunda, amesema kitendo kilichofanywa na askari huyo si kizuri kwani viongozi
wa klabu hizo wamekuwa wakitoa msaada mkubwa katika kuhakikisha timu hizo
zinapiga hatua kwenye soka hasa kudhibiti mianya ya wizi wa mapato uwanjani.




0 comments:
Post a Comment