Shamba la Selous Farming
Ltd lililopo Ifunda mkoani Iringa likimwagiliziwa kwa kutumia mtambo maalum
Kaimu mkuu wa mkoa wa Iringa ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Kilolo Gerald Guninita akizungumza na wamiliki wa shamba la selous.
Mmoja wa wamiliki wa shamba la selous bw Mack akitoa maelezo kwa wageni waliotembelea shamba hilo, kulia ni mkuu wa wilaya ya mufindi Evalista Kalalu
Meneja usindikaji wa kampuni ya usambazaji wa mbegu za mahindi na mtama SEEDCO
Tanzania limited, Venance Ndunga wakati wa ziara ya viongozi, wataalam, wakulima na wasambazaji wa pembejeo katika shamba la Selous Farming
Ltd lililopo Ifunda mkoani Iringa.
Wamiliki wa shamba la selous
Wageni mbalimbali wakiwa wamekaa kwenye majani wakati wakipata maelekezo kutoka kwa wataalamu wa seedco ambao wameshirikiana na ofisi ya mkuu wa mkoa kuandaa ziara hiyo
Wakati maenesho ya wakulima nane nane yakianza leo, jumuiya ya wakulima Tanzania imeanza kuchukua hatua kwa makampuni yanayodaiwa kuuza mbegu na mbolea feki.Meneja wa TFA mkoa wa Iringa Vitus Msofu amesema wamekua wakipokea malalamiko mengi kutoka kwa wakulima juu ya kuuziwa mbegu feki, jambo ambalo wameanza kulifanyia kazi kumaliza tatizo hilo.
Msofu ametoa kauli hiyo wakati wa ziara ya viongozi, wataalam, wakulima na wasambazaji wa pembejeo katika shamba la Selous Farming Ltd lililopo Ifunda mkoani Iringa
NAYE mkulima na mwekezaji wa shamba la Selous Farming Ltd Mark Tayloy amesema wataalam wa kilimo wamekua wakiwadanganya wakulima kuhusu matumizi ya mbolea aina ya minjingu hali iliyosababisha malalamiko kwa wakulima.
mack amesema mbolea ya minjingu haiwezi kufanya kazi kwa msimu unaoweka na badala yake manufaa yake huonekana msimu unaofuata hali iliyosababisha wakulima wengi kuilaumu serikali kusambaza mbolea isiyofaa, kumbe tatizo ni kwa wataalam wa kilimo na wanasiasa kushindwa kuwaambia ukweli wakulima au kutoijua mbolea hiyo vizuri.
Kwa upande wake mkulima aliyekuwepo kwenye msafara huo ameitaka serikali kuwasaidia wakulima kwa kuwaambia ukweli kuepuka hasara wanazopata.
0 comments:
Post a Comment