Main Menu

Monday, August 5, 2013

NEYMAR AGUNDULIKA KUWA NA UPUNGUFU WA CHEMBE HAI NYEKUNDU, MAN U YAITOSA OFA MPYA YA CHELSEA, UJERUMANI KATIKA KASHFA YA KUTUMIA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU MICHEZONI



Klabu ya Barcelona inayoshiriki ligi kuu ya Hispania imebainisha mchezaji Neymar da Silva anasumbuliwa na ugonjwa wa upungufu wa chembe hai nyekundu kwenye damu kwa lugha kitaalamu Anemia.

Neymar mwenye umri wa miaka 21 aligundulika ana tatizo la hilo wiki iliyopita wakati wa vipimo vya afya. Anemia ni tatizo linalosababisha uchovu kwa kiasi kikubwa na lina athiri maendeleo ya mchezaji.

Mkurugenzi wa michezo wa timu ya Barcelona Andoni Zubizarreta alithibitisha kuwa Neymar anasumbuliwa na tatizo hilo ingawa akasisitiza  mchezaji huyo anaendelea na matibabu chini ya jopo la matabibu wa klabu hiyo.

Neymar ambaye ni raia wa Brazil alijiunga na klabu ya Barcelona mwanzoni mwa mwezi wa sita kwa ada ya Euro milioni 57 akitokea klabu ya Santos.


Klabu ya Manchester united inayoshikiri ligi kuu ya England imekataa ofa ya pili ya timu ya Chelsea ya paundi milioni 30 wakitaka kumsajili mshambuliaji Wayne Rooney.

Manchester united wameshikilia msimamo wa kutomuuza Rooney mwenye umri wa miaka 27 ambaye anaonekana kupoteza furaha tangu mwishoni mwa msimu uliopita kutokana na kutokuwa na uhakika wa namba kwenye kikosi cha kwanza.

Rooney ambaye yupo ziarani nchini Sweeden na klabu yake ya  Manchester united wakijiandaa na msimu mpya wa ligi ameahidiwa kulipwa mshahara wa paundi laki mbili kwa juma kama atahamia Chelsea .

Mtendaji mkuu wa Manchester united Ed Woodward amesema pamoja na Rooney kubakisha mkataba wa miaka miwili klabu hiyo haina mpango wa kumpa mkataba mpya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England.

 

Gwiji wa zamani wa Uholanzi Johan Cruyff amesema nguvu ya pombe iliifanya wachezaji timu ya taifa ya Ujerumani magharibi kufanya vizuri kwenye mashindano kombe la dunia miaka ya 1960 mpaka 1970.

Cruyff amesema anayohadithi juu ya madawa ya kuongeza nguvu kuwekwa kwenye utayarishwaji wa pombe kitu kilichowasaidia wachezaji wa timu ya taifa ya Ujerumani magharibi kucheza  kwa nguvu bila kuchoka.

 Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na chuo kikuu cha Humboldt kilichopo Berlin kimegundua serikali ya Ujerumanini magharibi ilikuwa ikichochea makampuni ya pombe kuweka madawa ya kuongeza nguvu ili kuboresha afya za wanamichezo.

Cruyff anakumbuka miaka ya zamani hakukuwa na upimwaji wa madawa ya kuongeza nguvu michezoni kwasababu hiyo anafikiri ndio maana timu yao ya Uholanzi ilifungwa kwenye fainali ya kombe la dunia na timu ya taifa ya Ujerumani magharibi mwaka 1974.

Na MVP  Issa Maeda wa Ebony Fm

0 comments:

Post a Comment