Main Menu

Sunday, July 14, 2013

SHIRIKA LA NDEGE LA ASIANA KUKISHTAKI KITUO CHA TELEVISHEN CHA KTVU

 Siku ndege ya shirika hilo ilipolipuka huko san fransisco marekani wakati inatua
Shirika la Ndege la Asiana  limesema hii leo kwamba hadhi yake imeharibiwa kufuatia ripoti iliotangazwa katika televisheni ya Mjini San Fransisco ambayo ilitumia majina mabaya na ya kibaguzi kwa marubani wake wanne kufuatia ajali iliotokea hivi karibuni. 


Shirika hilo limesema linatafakari hatua za kisheria dhidi ya televisheni hiyo. 


Lakini halikufafanua ni hatua gani linapanga kuzichukua. 


Msoma Habari katika televisheni ya KTVU alisoma majina hayo hewani kisha akaomba radhi baada ya mapumziko. 


Marubani wa ndege hiyo waliohojiwa juu ya ajali hiyo na kundi la wachunguzi wa Marekani na Korea kusini wamerudi nchini mwao jana Jumamosi, na wanatarajiwa kufanyiwa mahojiano zaidi na maafisa nchini Korea Kusini.


Ndege nambari 214 ya kampuni ya Asiana ilianguka katika uwanja wa kimataifa wa San Frascisco Julai 6 na kuua watu watatu huku wengine wengi wakiachwa na majeraha.

Na dwswahili

0 comments:

Post a Comment