Rais Evo Morales wa Bolivia amesema mashirika ya kijasusi
ya Marekani yamedukua email au barua pepe za viongozi wa ngazi za juu wa
Bolivia.
Akizungumza Jumamosi, Morales amesema majasusi wa Marekani
wameweza kusoma barua pepe za maafisa wa ngazi za juu kabisa wa Bolivia.
Ameongeza kuwa ameshauriwa asitumie email na kufuatia ushauri huo
amefunga akaunti yake ya barua pepe.
Morales ameelezea wasi wasi wake
kuwa yamkini Washington ikatumia taarifa ilizopata katika barua pepe
hizo kupanga 'hujuma' dhidi ya nchi yake.
Mapema wiki hii Waziri wa
Mambo ya Nje wa Argentina Hector Timerman aliituhumu Marekani kuwa
imedukua barua pepe za maafisa zaidi ya 100 wa serikali ya nchi hiyo.
Hayo yanajiri katika hali ambayo viongozi wa Bolivia, Ecuador, Venezuela
na Nicaragua wametangaza kuwa tayari kumpa hifadhi Mmarekani Edward
Snowden ambaye alifichua kuwa mashirika ya ujasusi ya nchi hiyo hufanya
udukuzi kote duniani kwa kutumia mbinu ya kiteknolojia ya siri
kuchunguza mawasiliano ya simu ya watu, barua pepe na mawasiliano
mengine.
Na radio tehran swahili





0 comments:
Post a Comment