Main Menu

Wednesday, July 17, 2013

NINI MUSTAKABALI WA SIASA ZA TANZANIA NA VIKUNDI VYA GREEN GUARDS, RED BRIGADE NA BLUU GUARDS



Hakuna kitu kinachonipa mashaka sasa ninapotafakari siasa za Tanzania zinapopeleka usalama wa nchi yetu kama swala la hivi vikundi vyao vya "askari" vinavyofanya kazi chini ya vyama vya siasa (Militia groups affiliated under Political parties). Hapa nazungumzia Green Guards ya CCM na Red Brigade (kama sijakosea jina - naweza kurekebishwa) ya CHADEMA. Nimejiuliza maswali mengi sana hasa baada ya matukio ya hivi karibuni ambayo yanahusisha vikundi hivi kuhusika ikiwemo matukio kadha wa kadha huko Igunga pamoja na yaliyotokea jana huko Mwanza kama yalivyowasilishwa na baadhi ya members wa JF kuhusu Green Guard kupiga watu hadi kuwajeruhi huko Mwanza.

Naomba tujadili mwelekeo wa siasa ya Tanzania na kuwepo kwa vikundi hivi chini ya vyama kwa kuzingatia mambo yafuatayo.

  1. Hawa watu ni wakina nani? Je kuna sheria yoyote inayotoa uhalali wa kuwepo kwavyo?

  2. Je katiba za vyama vya siasa zinasehemu yoyote inayozungumzia kuwepo kwa vikundi hivi? Na kama ndiyo, je zimeanishaje majukumu ya vikundi hivi? Na je kuna uhalali wa kisheria unaotoa mwanya kwa vyama vya siasa kujianzishia vikundi kama hivi? Je inakubalika kuwepo kwa sheria ya namna hiyo?

  3. Je sheria ya vyama vya siasa inaruhusu kuwepo kwa vikundi hivi ndani ya vyama vya siasa? Kama sivyo je huu sio uvunjaji wa Sheria za Uanzishwaji wa Vyama vya siasa unaohitaji kuchukuliwa hatua? Au ndio tuseme "When the State is corrupt then the laws are most multiplied?"

  4. Je kuna wakati wowote ambao kuna kiongozi yoyote mwenye mamlaka ya usimamizi wa vyama vya siasa (Hapa namzungumzia Msajili wa Vyama vya Siasa ndugu John Tendwa) ametoa kauli ya kuzuia vikundi hivi? J e wale wenye mamlaka ya kusimamia usalama wa Taifa na Raia wake (Nazungumzia Jeshi la Polisi Tanzania na Jeshi la Wananchi wa Tanzania) wametoa kauli dhidi ya vikundi hivi ambavyo ni hatari kwa usalama wa Raia na Taifa kwa ujumla wake? Au ndio "Polisi Jamii" wenyewe?

  5. Je kuwepo kwa vikundi hivi ni ishara ya jeshi la polisi kushindwa kusimamia usalama wa shughuli za vyama vya siasa na ulinzi wa wanasiasa na kulazimisha kuanzishwa kwa vikundi hivi na vyama vya siasa ili kujihakikishia usalama?

  6. Je sisi kama Watanzania tunaona ni vema kwa vikundi hivi kuendelea kuwepo na kufanya kazi chini ya vyama vya siasa tena pasipo sheria halali wala majukumu yanayoeleweka? Viongozi wa vyama vya siasa mlioko hapa, bila kutafuna maneno, je mnadhani siasa yetu inahitaji sana vikundi hivi na wala sio polisi kusimamia yale ambayo vikundi hivi mmevianzishwa "kihunihuni"?


Niemuliza maswali haya kwa kuzingatia kuwa hapa tuna manguli wa mambo ya kisiasa wenye uzoefu wa siasa za kitaifa na kimtaifa, wanausalama wa Raia na Taifa na zaidi kuna viongozi wa Vyama vya siasa na wengine wakiwa kwenye Idara ya Uenzi na Itikadi ambao naamini kama hawatafungwa na ile kauli "Affection binds reason" wanaweza kutusaidia kupata picha ya vikundi hivi ambavyo kama sitapata msaada wa kuelewa kuwa vinaishi kihalali basi kwangu mimi ni "magenge ya wahuni" waliohalalishwa na "wahuni wenzao" wachache bila kuangalia mustakabali wa nchi hii.

ANGALIZO: Hapa sizungumzii unstructured group kama vile kundi la watu ambalo halikuwa limejipanga kufanya kitu fulani ila imetokea ghafla wakajikuta kuwa na common interest na kujiunga kufanya jambo fulani. Hapa nazungumzia kundi la watu ambalo limeandaliwa, limepewa jina, linafahamika na wanapatiwa hadi usafiri na nafasi ya kusimama mstari wa mbele au "kulinda usalama" huku wahusika wakiwa wanajua lipo kundi la namna hiyo na wakitolerate existence yavyo na utekelezaji wa "shughuli" zao. Na pia tujadili kwa mustakabali wa maendeleo ya taifa na sio kwa "maslahi"ya vyama vyetu vya siasa nikikopa msemo wa Invisible.


 

maoni ya mchangiaji

Kabla ya mwaka 1992, tulikuwa na chama kimoja tu (CCM). Pamoja na kuwepo kwa chama kimoja tu, kulikuwa na kitengo cha Green guards (Askari wa Kijani) kitengo kilichodaiwa kuwa ni kitengo cha kulinda chama. Kutoka mwaka 1992 ambapo vyama vingi viliruhusiwa na hasa kuanzia 1995, Chama cha CUF ndicho chama Kilicho kuwa na nguvu katika vyama vya upinzani nacho kikaunda kitengo cha Blue Guard(Askari wa bluu) kwa hoja hiyo hiyo ya kujilinda. Jana baada ya CHADEMA kutangaza kuimarisha kitengo chao cha Red Guard(Askari wekundu), wakidai ni kwa lengo hilo hilo la kujilinda, umeibuka mjadala mkali kwamba ni nini lengo la CHADEMA kuwa na kitengo hicho na tena wakiimarishe sawa sawa.
Kimsingi kuna maswali ya msingi ambayo watanzania tulitakiwa kujiuliza kabla hata ya kauli ya CHADEMA jana.Jambo la kushangaza ni kwamba hakuna alie hoji wala kushangaa kilichokuwa kinaendelea hadi jana CHADEMA walivyozungumzia suala la kujiimarisha ki ulinzi ndio watu waka gutuka hee!.Hebu tusaidianeni kutafakari mambo yafuatayo.

1. Katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ina kataza mtu,chama au taasisi yoyote kuunda jeshi au chombo chenye muelekeo wa kijeshi “Para-millitary groups” ispokuwa serikali yenyewe. Kwa mfano; Katika sura ya tisa ya Katiba; inaeleza ;147.-(1) “Ni marufuku kwa mtu yoyote au shirika lolote aukikundi chochote cha watu, isipokuwa Serikali kuunda au kuweka Tanzania jeshi la aina yoyote” .Sasa pamoja na kifungu hiki cha katiba; CCM, CUF na sasa CHADEMA wana vikosi vya ulinzi ndani ya chama. Je inamaana ni ukiukaji wa katiba? Ikiwa ni ukiukaji wa katiba;
(a) Kwa nini CCM waliamua kukiuka,CUF walivyowaona nao wakakiuka na sasa CHADEMA nao wanakiuka?
(b) Ni kwa nini hili linaonekana sasa wakati CHADEMA imetangaza kujiimarisha katika kujilinda?
2. CCM ndiyo imetawala kwa kipindi chote toka tupate uhuru. Mwenyekiti wa CCM huwa ndio anakuwa Rais katika kipindi chote. Rais huwa ndio Amiri jeshi mkuu (wa majeshi yote) kwa mujibu wa katiba.Je! Green guard wana kazi ya kuilinda CCM dhidi ya nani?
3. Matendo yaliyowahi kufanywa na Green guards (CCM) tumeshawahi kuyaona, yaliyo fanywa na Blue Guard (CUF) Tumeshawahi kuyaona.Je;kwa vile yanavyoonekana ni matendo sahihi? Kama si sahihi, tumeshawahi kuyakemea?
4. Kazi za Jeshi la Polisi ni kulinda raia (wote bila kujali siasa) na mali zao, kulinda amani, kuhakikisha sheria zinafuatwa,kuzuia na kupeleleza uhalifu na kukamata uhalifu.Sasa;

(i) Je! CCM wana imani na jeshi la polisi?

(a) kama wana imani na Polisi kwa nini wameunda kikundi jeshi ndani ya chama kwa hoja ya kujilinda?

(b) Kama hawana imani; kwa kuwa wao ndio wenye serikali, kwa nini wasiliboreshe jeshi la polisi kinyume chake wanaanzisha vikundi vingine nyume ya pazia?
(ii)Kwa sasa CHADEMA wanadai hawana imani na Polisi na hata kudai kwamba wanaowashambulia wakati mwengine ni Polisi waliotumwa,Ikiwa ndio hivyo;kwa kuwa polisi ndio waliotakiwa wa hakikishe ulinzi lakini hawafanyi hivyo, na CHADEMA hawawezi kuwalazimisha kufanya hivyo,

(a)Waachetu waendelee kutokuwa na ulinzi na hatimae waendelee kudhuriwa? Au

(b)Waunde kikundi ulinzi (hata kama ni kinyume na katiba) lakini wajihakikishie usalama na hasa ukizingatia wa kabla yao walishaunda?

5. Kwa kuwa CHADEMA Wanaamini anaye washambulia mara nyingi ni Polisi (kwa maagizo ya viongozi wa CCM), Na sasa wanatangaza kuunda kikosi ulinzi kwa ajili ya kujilinda, na wakati huo huo CCM nayo ilishakuwa na vikosi vya Green guards toka siku nyingi na kazi zake mnazijua. Je;tutaraji,
(a) Kuona vikosi vya ulinzi vya Chadema vikiwadhibiti washambuliaji (ambao wanaweza kuwa Polisi)? Ikiwa ndio hivyo basi, na Polisi nalo ni jeshi tena halali na lenye zana kali za kivita tutaraji nini?
(b) Tutarajie kuona CHADEMA wakiwadhibiti wanaodhani wanataka kuwadhuru (yaani CCM) Na kwa kuwa CCM nao tayari wana vikosi vya Green Guard ambavyo mnavijua, Tutarajie mambano kati ya“ Two paramilitary groups”? (kwa kuwa vikundi ulinzi wakati Fulani huwajibika kutumia nguvu!).
Ushauri; Namshauri Rais kikwete aiangalie tena nchi hii. Ageuze uzo wake tena na tena azitizame mbio hizi zinazoendelea. Asichukulie mzaha hata kidogo kwa kudhani kuwa ni kuinusuru CCM kumbe mwishowe itakuwa dhahama kwa Taifa. Namsi Mh.Rais akumbuke kuwa kwa yeyote anaeshambuliwa. Ana machaguo mawili tu. Aache auawe, au ajikinge kwa njia anayoweza (hata kama ni kupambana).
Jambo la afya ambalo ni muhimimu kwa Rais; ni kukufanya juu chini kuhakikisha analirudisha tena jeshi la Polisi kuwa ni jeshi la watu (umma) na hivyo kufanya watu wote kuwa na imani nalo tena. Kwa kufanya hivyo kakuna Chama kitakacho fikiaria kuhusu habari za kujilinda . Hili linawezekana kwa kutoa amri moja tu ya kulitaka jeshi lisipendelee chama chochote hata kama ni CCM.

NA JAMIIFORUM

0 comments:

Post a Comment