Main Menu

Tuesday, June 4, 2013

WAHUDUMU WA HOTEL WAPEWA MAFUNZO MKOANI IRINGA ILI KUBORESHA SEKTA HIYO


 washiriki wa mafunzo kwa wahudumu wa hotel katika hotel ya M.R mkoani iringa.
mkurugenzi wa veta kanda ya nyanda za juu kusini monica mbelle aliyesimama akiongea na wafanyakazi wa M.R hotel
afisa utalii wa tanapa kanda ya kusini risala kabongo akizungumza na washiriki wa mafunzo

                  washiriki wakisikiliza maelezo kwa umakini




Ili kuongeza ushindani katika utoaji huduma kwenye sekta ya hotel na kuwavutia watalii, Wamiliki wa Hotel mkoani  Iringa wametakiwa kuwaajiri wafanyakazi wenye sifa na kuwapa mafunzo ya mara kwa mara.

Akizindua mafunzo kwa wafanyakazi wa hoteli ya M.R iliyopo mkoani iringa kama mkakati wa kuboresha huduma za hotel, mwenyekiti wa bodi ya VETA kanda ya kusini, Kabaka Ndenda amesema ni vigumu kufanya kazi nzuri bila kuwapa wafanyakazi mafunzo ya mara kwa mara.


Kwa upande wake mkurugenzi veta  kanda ya nyanda za juu kusini, Monica Mbelle amewataka wananchi kutowapeleka vijana wao kwenye vyuo ambavyo havijasajiliwa ili kuwaepusha kupata elimu ambayo haitatambulika pindi waendapo kutafuta ajira.


Naye afisa utalii wa Tanapa kanda ya kusini Risala Kabongo amewataka wahudumu wa Hotel kujitambua kuwa ni watu muhimu katika kukuza utalii wa kusini na kujijengea heshima wao wenyewe.


Mafunzo hayo  ya wiki moja yameratibiwa  kwa ushirikiano wa Veta na M.R Hotel yakiwa na lengo la kuboresha huduma za hotel  mkoani  Iringa baada ya utafiti uliofanywa na chuo cha ufundi VETA katika hotel tano na  kubaini upungufu katika utoaji huduma.

0 comments:

Post a Comment