Mvutano wa kimataifa unaendelea kuongezeka dhidi ya serikali ya Korea Kaskazini kuhusiana na mpango wake wa nyuklia. Korea Kaskazini imesema kuwa itaanzisha tena operesheni za kinu cha nyuklia cha Yongbyon.
Kinu hicho kilifungwa mwaka
wa 2007 kama sehemu ya mazungumzo ya kimataifa ya kusimamisha mipango ya nyuklia, ambayo yamekwama tangu wakati huo.
Marekani imelijibu vikali tangazo hilo ikilitaja kuwa lisilokuwa na msingi na lisilokubalika.
Rais wa Korea Kusini Park Geun-Hye
Waziri wa Mambo ya Nchi za Kigeni wa Marekani John Kerry amekutana jana na mwenzake wa Korea Kusini mjini Washington na akaeleza msimamo wa Marekani akisema kuwa, hatua aliyoichukua rais wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un ni ya uchochezi na hatari, na serikali ya Marekani haitaikubalia Korea Kaskazini kutengeneza silaha za nyuklia.
Amesema Marekani itafanya kila iwezalo kujilinda pamoja na washirika wake Korea na Japan.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ambaye pia anatokea Korea Kusini amezungumzia hali hiyo akisema kuwa vitisho vya silaha za nyuklia siyo jambo la mzaha.
0 comments:
Post a Comment