Mahakama nchini Afrika Kusini imemruhusu Oscar
Pirstorius kusafiri nje ya nchi, na hivyo kumlegezea
masharti makali ya dhamana, baada ya kushtakiwa kwa
mauaji ya mpenzi wake. Pistorius alikata rifaa dhidi ya
mlolongo wa masharti ya dhamana ambayo alisema
hayakuwa ya haki na wala hayakutakiwa.
Jaji Bert Bam wa mahakama ya juu ya mjini Pretoria
amesema uamuzi wa awali wa hakimu kumuamrisha
Pistorius kukabidhi hati yake ya kusafiria haukuwa
sahihi.
Hata hivyo, Pistorius atalaazimika kuwasilisha
mpango wake wa safari kwa upande wa mashtaka angalau
wiki moja kabla ya kusafiri, na kukabidhi tena hati yake
ndani ya masaa 24 baada ya kurejea kutoka safarini.
Pistorius hakuwepo mahakamani wakati uamuzi huo
unatolewa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment