Mkuu wa mkoa wa Manyara Dokta, Joel Bendera
ameipongezs TFF kwa kuandaa mashindano ya ya Taifa ya vijana wenye umri chini
ya miaka 13 (U-13), na maandalizi ya timu hiyo kwa ajili ya kuwania kufuzu
kwa fainali za Afrika za vijana chini ya miaka 17 zitakazofanyika mwaka 2019
nchini Tanzania.
Bendera amesema hiyo ndiyo njia sahihi ya
kuelekea kwenye mafanikio pia amepongeza juhudi za Chama cha Soka mkoa wa
Manyara na TFF kwa kuandaa kozi za makocha na waamuzi, akisema huo ndiyo
uwekezaji mkubwa katika maendeleo ya soka mkoani Manyara.
Aidha aliwaasa makocha kutumia mbinu za
kisasa za ufundishaji soka walizozipata kwenda kuendeleza vipaji vya wachezaji
watakaowafundisha.
Pia Bendera amewahakikishia wakazi wa Manyara
atahakikisha wanaandaa vipaji vitakvyowawezesha kuwa na timu bora
itakayowakilisha mkoa wa Manyara.
0 comments:
Post a Comment