Main Menu

Wednesday, July 1, 2015

TAIFA STARS KUIFUATA UGANDA KESHO



 
Timu ya taifa ya Tanzania taifa stars inatarajiwa kuondoka kesho kuelekea nchini Uganda kwa ajili ya mchezo wa kufuzu kwa michuano ya afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani CHAN.

Stars inaondoka kesho ikiwa na deni la magoli matatu kwa bili iliyofungwa katika mchezo wa awali uliofanyika visiwani Zanzibar.

Nahodha wa timu hiyo ambaye anatibia jeraha la kichwa Nadir Haroub amesema mabadiliko ya kocha yameleta morali katika kikosi hicho.

Kuhusu jeraha alilonalo nahodha huyo, dr wa Stars Bruno Faragha amesema mpaka siku ya mchezo atakua fiti.

Ili Stars isonge mbele inahitaji ushindi wa mabao manne kwa bila, na kama itafanikiwa itakabiliana na Sudan katika hatua ya mwisho ya mtoano.

0 comments:

Post a Comment