Rais wa Baraza la Vyama vya Soka kwa nchi za
Afrika Mashariki na Kati, Leodgar Tenga leo ametangaza kuanza kwa michuano ya
kombe la Kagame itakayoanza kutimua vumbi Julai 18, 2015 na kumalizika Agosti 2
mwaka huu jijii Dar es salaam.
Akiongea na waandishi wa habari leo katika
ofisi za TFF zilizopo Karume, Tenga ameishukuru serikali ya Tanzania na TFF kwa
kukubali kuwa wenyeji wa michuano hiyo mikubwa, vyombo vya habari na wapenzi wa
mpira wa miguu nchini kwa sapoti yao na kuipokea kwa mikono miwili michuano
hiyo.
Lengo la CECAFA ni kuona vilabu vya ukanda
huu vinapata nafasi ya kucheza michezo mingi na kujiandaa kwa ajili ya michuano
ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Naye Rais wa TFF, Jamal Malinzi amewashukuru
CECFA kwa kuipa Tanzania uenyeji huo na kuahidi TFF itahakikisha michuano hiyo
inafanya nchini katika hali ya amani na usalama toka mwanzo mpaka mwisho wa
michuano hiyo.
Timu zilizothibtisha kushiriki michuano hiyo
ni Yanga, Azam (Tanzania), APR (Rwanda), Gor Mahia (Kenya), Telecom (Djibout),
KMKM (Zanzibar), Khartoum-N (Sudan), Al Shandy (Sudan) LLB AFC (Burundi),
Heegan FC (Somalia), Malakia (Sudani Kusini), Adama City (Ethipia) na KCCA
(Uganda).
Wakati huo Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholaus
Musonye ametangza ratiba ya michuano ya Kombe la Kagame itakayoanza kutimua
vumbi Julai 18, 2015 jijini Dar es salaam ikishirikisha timu 13 kutoka nchi
wanachama wa CECAFA.
Mechi ya ufunguzi tarehe 18 Julai, 2015
Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam itashuhudia wenyeji Yanga SC wakicheza na
Gor Mahia ya Kenya, huku APR ya Rwanda ikicheza na Al Shandy ya Sudan na KMKM
ya Zanzibar wakifungua dimba na Telecom ya Somalia.
Ratiba ya michuano hiyo imeziweka timu hizo
katika makundi matatu ambapo kundi A lina timu za: Yanga (Tanzania), Gor Mahia
(Kenya), Telecom (Djbiout), KMKM (Zanzibar) na Khartoum-N (Sudan)
Kundi B: APR (Rwanda), Al Shandy (Sudan), LLB
AFC (Burundi) na Heegan FC (Somalia), Kundi C: Azam FC (Tanzania), Malakia
(Sudan Kusini), Adama City (Ethiopia) na KCCA (Uganda)
Timu tatu zitakazoshika nafasi ya juu kutoka
kundi A, timu mbili za juu kutoka kundi B & C, na mshindi mwenye wastani
mzuri kutoka kundi B & C zitaingia katika hatua ya robo fainali.
0 comments:
Post a Comment