Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF leo
limezindua jezi mpya za timu za Taifa, zitakazokuwa zikitumika na timu za Taifa
katika michuano mbali mbali itakayokua inazikabili.
Uzinduzi huo wa jezi mpya uliofanyika
katika ukumbi wa Kilimanjaro jengo la Golden Jubilee uliambatana na uziduzi wa
tovuti mpya ya shirikisho, uliongozwa na mgeni rasmi Mh. Said Mtanda, mbunge wa
jimbo la Mchinga na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya jamii.
Katika uzinduzi huo, kulizunduliwa jezi
aina tatu, ambazo ni jezi za ugenini, jezi za nyumbani na jezi zitakazokuwa
zikitumika kwa ajili ya mazoezi.
0 comments:
Post a Comment