Mh Said Mtanda Mbunge
wa Jimbo la Mchinga na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii
Mzee Said el Maamry Mwenyekiti Msataafu wa FAT
Ndugu Leodeger Tenga Mjumbe wa Kamati ya utendaji ya CAF
na Rais mstaafu wa TFF
Ndugu wageni waalikwa
Ndugu waandishi wa habari
Mabibi na mabwana
Salam aleikum.
Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa
kutufikisha hapa leo na kwa mafanikio mbali mbali ambayo tumekuwa
tukiyapata.Ninakushukuru sana ndugu mgeni rasmi kwa kuacha shughuli zako kuja
kujiunga nasi asubuhi hii katika shughuli hii.
Ndugu mgeni rasmi,tarehe 08 oktoba 1964 Tanzania ilipata
uanachama rasmi wa shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA. TFF tuliona jambo
zito kama hili hatuwezi kuliacha lipite hivi hivi.Hivyo mwaka jana tuliamua
kuenzi maadhimisho ya miaka 50 ya kujiunga na FIFA kwa kufanya mambo
mambo matatu makubwa.
La kwanza ni kutoa vyeti maalum kwa watu binafsi na
taasisi mbali mbali kwa kutambua mchango wao uliotukuka katika kuendeleza mpira
wa miguu Tanzania.
Leo hii ndugu mgeni rasmi tutakuomba ukabidhi vyeti hivi
kwa wawakilishi wa makundi kadhaa kwa niaba ya wenzao.Makundi haya ni pamoja na
viongozi wa kitaifa wastaafu,mawaziri wa michezo wastaafu,viongozi waliopita wa
TFF?
FAT,wakurugenzi wa idara ya michezo,wenyeviti na makatibu
wa baraza la michezo la taifa,Timuya Taifa iliyocheza fainali za Afrika mwaka
1980,waamuzi,makocha,wachezaji wa timu ya Taifa na watangazaji mahiri wa
michezo.Jumla tumetunuku vyeti 194.
Kiuhalisia idadi hii
ni ndogo sana ukilinganisha na wingi na uzito wa michango ya wadau mbali mbali
wa mpira katika miaka 50 iliyopita.
Tunaomba Watanzania
wenzetu watuelewe katika hili kuwa hawa tutakaowatunuku vyeti hivi ni
wawakalilisha wa wadau wote wa mpira Tanzania.
Ninaomba tusimame kwa muda mfupi tuwaombe ewadau wenzetu
na viongozi wa mpira wa miguu ambao wako katika orodha hii na wametangulia
mbele ya haki.
Ndugu mgeni rasmi katika kuenzi miaka 50 ya Tanzania
kujiunga na FIFA leo hii pia tutatoa mchango wa fedha kwa makundi yenye
mahitaji katika jamii.
Pesa hizi zinatokana na makusanyo mbali mbali ikiwemo
makusanyo ya mechi ya ngao ya hisani ifanyikayo kila mwaka. Makundi haya ni pamoja
na walemavu wa viuongo,walemavu wa ngozi na wasioona.
Kitendo hii ni moja ya juhudi za TFF kurudisha katika
jamii kile tunachokusanya. Kila kundi litapewa shilingi milioni tano na
tunaendelea kupokea maombi toka makundi mbali ya kijamii na tukiyapitisha
tutaendelea kugawa fedha hizi.
Jambo la tatu tutakalolifanya leo litakuwa ni kuzindua
rasmi tovuti mpya ya TFF (www.tff.or.tz). Tumeamua kufanya jamabo hili
katika kuenzi miaka hamsini ya kujiunga na FIFA ili kutoa msisitizo kuwa sasa
TFF na sisi tunajiunga Na kuendeleza mpira kisasa kulingana na teknolojia
iliyopo.
Kupitia tovuti hii
wadau wa mpira watapata fursa ya kuhabarishwana kuelimishwa nkuhusu masuala
mbali mbali yahusuyo mpira wa miguu.
Tovuti hii itakuwa
pia na sehemu ya kumbu kumbu (archive) zihusuzo historia ya mpira wa miguu na
matukio mbali mbali katika historia ya mpira wetu.
Tunaomba wadau wenye
kumbu kumbu mbali za mpira kama picha,takwimu,vipande vya magazeti ya zamani na
kadhalika mtuletee ili viingizwe katika tovuti yetu.
Tunaamini tovuti hii
itakuwa ndio chanzo kikuu cha taarifa na rekodi mbali mbali za sasa na za
zamani zihusuzo mpira wa miguu.
Ndugu mgeni rasmi shughuli ya leo tutaihitimisha kwa
kuzindua jezi mpya ya timu ya Taifa. Jezi hizi zitakuwa ni mbili moja ya
ugenini na nyingine ya nyumbani.Tunawapongeza watanzania wote walioshiriki
katika kubuni jezi na mwisho tuliunganisha ubunifu tofauti na kupata jezi
itakayozinduliwa leo.
Ubunifu huu tayari umetafutiwa hati miliki Brela hivyo
TFF tutalinda hakii hii kwa kuwakamata na kuwafikisha mbele ya vyombo vya
sheria wale wote watakaodiriki kuchapisha na kuuza kwa magendo jezi
hizi.Utaratibu unafanyika kumpata msambaji mmoja halali atakayesambaza jezi
hizi nchini kwa ajili ya wapenzi wa mpira wa miguu.Ukinunua jezi hii utakuwa
umechangia maendeleo ya mpira wa miguu.
TFF inawashukuru na kuwapongeza sana Tanzania
Breweries ltd ambao ndio wazalishaji wa bia ya Kilimanjaro Lager kwa sapoti
wanayoitia kwa timu ya Taifa na kutuwezesha kubuni na kuzalisha jezi
hizi.Tunawashukuru sana.
Ndugu mgeni rasmi ninaomba nimalizie kwa kuzungumzia kwa
kifupi program yetu ya mpira wa vijana.kwa kutambua umuhimu wa kuendeleza soka
la vijana TFF tumejipanga vilivyo kwa mpambano wa hatua za awali za kucheza
fainali za vijana za Afrika umri chini ya miaka 17 mwaka 2017.
Mechi za ufaulu zitafanyika kati kati ya mwaka 2016.TFF
tayari tumeunda kikosi cha awali cha vijana chini ya umri wa miaka 15 kujiandaa
na michuano hii.Kikosi hiki kimetokana na michuano ya copa coca cola ya mwaka
jana.
Tunapenda tuchukue fursa hii kumshukuru Rais Dr Jakaya
Mrisho Kikwete kwa kufanikisha nchi yetu ya Tanzania,kwa mara ya kwanza katika
historia ya nchi hii,kupata uenyeji wa fainali za Afrika. Shirikisho la mpira
wa miguu Afrika CAF limeipatia Tanzania uenyeji wa fainali za Afrika za vijana
umri chini ya miaka 17 mwaka 2019.
Tunaomba Serikali itushike mkono katika hili ili tuweze
kuandaa mashindano mazuri.Lakini haitakuwa vyema Tanzania kuandaa mashindano
mazuri lakini tukatolewa hatua ya makundi.Siku ya jumapili tarehe 07/juni TFF
tutazindua mashindano ya taifa ya vijana umri chini ya miaka 13 mjini mwanza.
Wachezaji bora wa mashindano haya ndio wataunda
kikosi cha awali cha Taifa kwa ajili ya kushiriki fainali za Afrika watoto umri
chini ya miaka 17 mwaka 2109.
Tunaomba Serikali pamoja na wadau wote tushirikiane
katika kukilea kikosi hiki ili mwaka 2019 tuwe na timu nzuri.
Tunamshukuru Mh Dr Fennela Mukangara na wizara nzima ya
habari vijana utamaduni na michezo kwa ushirikiano wanaotupatia katika hatua
hizi na katika shughuli nyingine za kuendeleza mchezo wa mpira wa miguu.
Ndugu mgeni rasmi ninaomba sasa nikukaribishe uhutubie
hafla hii na pia utuongoze katika shughuli zitakazofuata.
Ahsate sana
0 comments:
Post a Comment