TFF imepokea kwa
masikitiko makubwa taarifa za mgogoro wa kimkataba kati ya Mchezaji Ramadhani
Singano wa klabu ya Simba.
TFF imeagiza
mwakilishi wa klabu ya Simba pamoja na mchezaji wa Simba wafike ofisi za TFF
siku ya Jumanne tarehe 09/06/2015 kwa mazungumzo.
Kila upande umetakiwa
uje na vielelezo vyake.
Katika kipindi hiki
cha kuelekea kwenye mazungumzo,TFF inaziasa pande zote mbili zijiepushe na
kutoa matamko yanayoweza kuchochea hali ya kutoelewana na kuamsha hisia mbaya
katika familia ya mpira wa Miguu Tanzania.
0 comments:
Post a Comment