Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars)
inayodhamini na kampuni ya bia ya Kilimanjaro, leo imeanza mazoezi katika
uwanja wa Addis Ababa zamani ukifahamka kama (Haille Sellsie) uliopo
jijini Addis Ababa kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri utakaopigwa Juni 14,
jijini Alexandria.
Stars ambayo iliwasili jana jioni jijini
Addis Ababa imefikia katika hoteli ya Debre Damo iliyopo eneo na 22 Mazoiria
ambapo itakaa kambi kwa kipindi cha wiki moja kujiandaa na mchezo dhidi ya
Mapaharao.
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa Stars Mart Nooij
amesema anashukuru vijana wake wamefika salama, na wapo katika hali nzuri,
anaamini wiki moja ya maandalizi nchini Ethiopia itasaidia kikosi chake kuwa
fiti ajili ya mchezo.
Akiongelea kuhusu kambi, kocha Nooij amesema
kwa kuwa mji wa Addis Ababa upo katika ukanda wa juu( mita 2000 kutoka usawa wa
bahari), kambi ya mazoezi itakua nzuri kutokana na wachezaji kufanya mazoezi
katika hali hiyo na kwenda kucheza katika ukanda wa kawaida.
Kuhusu hali ya hewa ni nzuri kwani baridi
iliyopo kwa sasa Addis Ababa ni ya kawaida, hivyo haitaweza kuwasumbua
wachezaji katika maandalizi ya mchezo dhidi ya Misri.
Mchezo kati ya Misri na Tanzania unatarajiwa
kuchezwa katika jiji la Alexandria ambalo lipo eneo la bahari ya Mediteranian.
0 comments:
Post a Comment