Sakata la kujiuzulu kwa Rais wa FIFA Joseph ‘Sepp’Blatter
limechukua sura mpya Kufuatia vyombo mbalimbali vya dola kuanza kazi ya
kumchunguza Rais huyo anayehusishwa na ubadhilifu wa fedha za FIFA au rushwa.
Tayari shirika la ujasusi la Marekani FBI na baadhi ya
waendesha mashtaka wa nchi hiyo wameanza kumchunguza Blatter kuona kama ana
hatia na kashfa za rushwa za FIFA.
Mmoja kati ya watu wa karibu wa Blatter Walter Gagg
anasema kuwa “Blatter alikuwa katika hali ya kawaida sana kwa siku ya jumatatu
lakini hali yake ilibadilika siku ya jana(Jumanne) kutokana na ripoti za vyombo
vya Habari kuhusu kuhusika kwake na rushwa.”
Wakati hayo yakiendelea,wachunguzi wa mambo wanasema kuwa
ripoti ya kurasa arobaini ya ushahidi wa mmoja kati ya wajumbe wa zamani kamati
ya utendaji ya FIFA ‘Chuck Blazer’ inaweza kuibua mambo mengi kuhusu Shrikisho hilo.
Kitendawili kikubwa ni ani atakuwa mrithi wa Blatter kati
ya Michel Platini, Prince Ali Bin Hussein, David Gill, Luis
Figo na Michael Van Praag.
0 comments:
Post a Comment