Hatimaye klabu ya Real Madrid imemteua kocha Rafael
Benitez kuwa kocha wao mpya kwa mkataba wa miaka 3.
Rafael Benitez anachukua nafasi ya kocha mtaliano Carlo
Ancelotti aliyetimuliwa mwishoni wa msimu huu wa La Liga baada kushindwa
kuchukua taji hata moka katika msimu huu.
Kocha huyo ameifundisha klabu ya Napoli ya nchini Italia
baada ya kudumu nayo kwa misimu mitatu na kuiongoza timu hiyo kushika nafasi ya
tano msimu huu katika Ligi kuu ya soka nchini Italia.
Mtandao wa klabu ya Real Madrid uliandika taarifa kuwa
“Rafel Benitez amepewa mkataba wa miaka mitatu leo siku ya jumatano ya tarehe 3
mwezi wa sita mwaka 2015.
0 comments:
Post a Comment