Fainali ya kwanza Ligi ya mpira wa kikapu ya nchini
Marekani inategemewa kufanyika alfajiri ya kesho kwa mchezo mkali na wa
kusisimua kati ya Cleveland Cavaliers na Golden State Warriors.
Cleveland Cavaliers ni mabingwa wa kanda ya mashariki
mara baada ya kuwatoa Atlanta Hawks huku Golden State Warriors wakiwa mabingwa
wa kanda ya magharibi baada ya kuwatoa Houston Rockets.
Cleveland Cavaliers hajawahi kushinda taji la NBA ingawa
wameshawahi kufika fainali za NBA mwaka 2007 pale Lebron James na wenzake
walipoiongoza Cavaliers kucheza fainali.
Katika mchezo huo wa fainali Cavaliers wakafungwa
na timu ya San Antonio Spurs.
Jiji la Cleveland halijawahai kushinda taji lolote kwa
takribani miaka 51, Cleveland kama kawaida itakuwa na nyota wake katika mchezo
wa fainali kama Lebron James, Kyle Irving, Kevin Love, Matt Delavedova na J.R
Smith.
Kwa upande wa Golden State Warriors walichukua ubingwa wa
NBA mwaka 1975 na ni miaka 40 imepita tangu wachukue ubingwa huo wa NBA.
Timu hii inajivunia uwepo wa wachezaji wake ambao
wamecheza pamoja muda mrefu katika timu hiyo tangu mwaka 2009.
Wachezaji hao ni Stephen Curry, Klay Thompson, Harrison
Barnes na Draymond Green.
0 comments:
Post a Comment