Simba sports club
Taarifa
kwa vyombo vya habari
Kikao
cha kamati ya utendaji ya club ya simba kilichokutana jana tarehe 10/06/2015,
pamoja na mambo mengine kilijadili suala la mchezaji wa Simba Ramadhan Yahya
Singano na kuamua yafuatayo:
Kwakuwa Mchezaji Ramadhan Yahya Singano alivunja makubaliano yaliyoamuliwa katika kikao cha pamoja kati ya club ya Simba, mchezaji mwenyewe, sputanza na secretarieti ya shirikisho la mpira wa miguu nchini(TFF) ya kutozungumzia yaliyojadiliwa na kupendekezwa kwenye kikao kwa kuyazungumza kwenye vyombo vya habari kwa kusema yeye ni mchezaji huru,
Klabu ya simba imeamua kutokufanya mazungumzo na mchezaji huyo kwa sasa kwa kuwa bado ina mkataba naye ambao utaisha 01/07/2016.
Hata hivyo Klabu itakuwa tayari kufanya nae mazungumzo pindi muda muafaka utakapofika kwa mujibu wa kanuni na taratibu za mikataba.
Ni
matarajio yetu mchezaji Singano ataheshimu maamuzi hayo na mkataba ambao pia
upo TFF na kwenye mtandao TMS.
Imetolewa
na Evans Aveva
Rais
Simba Sports Club
Rais
Simba Sports Club
0 comments:
Post a Comment