Bodi ya ligi Tanzania kwa kushirikia na wadhamin wa ligi
hiyo kampuni ya Vodacom usiku huu imetoa tuzo kwa washindi mbalimbali wa ligi
hiyo.
Kulikua na vipengele vitano vilivyokua vinashindaniwa
ambavyo ni mchezaji bora wa msimu, golikipa bora, mwamuzi bora, timu yenye
nidhamu na kocha bora.
Nafasi ya bingwa na zile nafasi zingine za juu zenyewe
zilishajulikana kama ilivyokua na mfungaji bora.
Pamoja na kulalamikiwa tangu pale walipotajwa majina ya
washiriki, leo bado bodi ya ligi imeendelea kuwashangaza watu kwa kumteua
mbwana makata kuwa kocha bora wa ligi kuu msimu uliopita.
Makata alikua anachuana na kocha wa yanga hans van pluijm
pamoja na aliyekua kocha wa Simba Kopunovic.
Wazazi wa Simon wakipokea tuzo za mwanae ambaye yupo na timu ya taifa Ethiopia.
Tuzo ya mchezaji bora imekwenda kwa Simon Msuva baada ya
kuwaangusha Mrisho Ngassa, na Mohamed Husein Shabalala.
Kipa bora amepewa shaban Hassan Kado, wakati timu yenye
nidhamu imepewa mtibwa sugar.
Mwamuzi wa msimu ni Israel Mujuni Nkongo.
0 comments:
Post a Comment