Msimu wa Ligi mbalimbali unategemewa kumalizika hapo
kesho ikiwa ni safari ya miezi takribani kumi ya ushindani katika Ligi hizo.
Ligi ambazo michezo yake inamalizika hapo kesho ni pamoja
na Ligi ya Ujerumani Bundesliga, Ligi ya Hispania La Liga na Ligi ya Ufaransa
maarufu kama Ligue 1.
Ligi ya Ujerumani itamalizika kesho kwa michezo saba
kupigwa katika viwanja saba tofauti.
Bingwa wa Ligi hiyo kishajulikana ambaye ni Bayern Munich
lakini timu zipi zitashuka daraja bado ni kitendawili kinachohitaji kuteguliwa
hapo kesho.
Timu za Paderborn na Hamburg SV zinaonekana zimeshashuka
daraja kimahesabu ingawa michezo ya mwisho hapo kesho itaamua pia.
Lakini bado mustakabali wa timu nyingine ya tatu toka
mkiani ambayo itacheza mtoano na timu iliyoshika nafasi ya tatu ya Ligi ya
daraja la pili ya Bundesliga haijajulikana bado.
Timu za VFB Stuttgart,Hannover 96 na Freiburg zinapambana
kutocheza hatua ya mtoano ya kubaki katika Ligi ya Bundesliga msimu ujao.
Nchini Ufaransa pia Ligi yao itamalizika siku ya kesho.
Tayari PSG ndio mabingwa wa Ligi ya Ufaransa kwa msimu
huu ikiwa ni mara ya tatu mfululizo kwa PSG kuchukua Ligi Kuu ya Ufaransa
maarufu kama French Ligue 1.
Mchezaji bora wa msimu huu kwa Ligi ya Ufaransa ni
Alexandre Lacazette wa Olympique Lyon huku tuzo ya mchezaji bora chipukizi
ikienda kwa Nabir Fekir wa Olympique Lyon pia na tuzo ya golikipa bora ikienda
kwa Steve Mandanda wa Olympique Marseille.
Tuzo ya kocha bora wa msimu imeenda
kwa kocha wa PSG Laurent Blanc.
Wakati Ligi za Ufaransa na Ujerumani zikifikia tamati
hapo kesho,Ligi ya Hispania maarufu kama La liga pia itafikia tamati hapo kesho pia.
Klabu ya Barcelona ndio mabingwa wa Hispania kwa msimu
huu wa mwaka 2014/15.
Maswali ni mengi
ya nani atachukua tuzo ya mchezaji bora wa Ligi hiyo kwa msimu huu?Lakini vipi
kwa tuzo ya mfungaji bora wa Ligi hiyo
(Pichichi) itaenda kwa Ronaldo au Messi?
Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo
anaonekana kuwa katika nafasi nzuri ya kuwa mfungaji bora wa Ligi hiyo.
Kwa sasa Ronaldo ana magoli 45 akifuatiwa na Messi mwenye
magoli 41.Tusubiri michezo ya mwisho ya La Liga hapo kesho
Ligi Kuu ya soka nchini England yenyewe itafikia tamati
siku ya Jumapili huku Ligi ya Italia ikisogea kwa juma moja mbele ili
kumalizika.
0 comments:
Post a Comment