Shirikisho la Mpira wa
Miguu nchini TFF, limetangza viingilio vya mchezo wa siku ya jumapili kati ya
Taifa Stars (Tanzania) dhidi ya The Flames (Malawi) utakaochezwa kwenye uwanja
wa CCM Kirumba jijini Mwanza kuwa ni tsh. 5,000 mzunguko na tsh. 12,000 kwa
jukwa kuu.
Kuelekea mchezo huo wa
jumapili kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na
Bia ya Kilimanjaro, kimeendelea na mazoezi katika Uwanja wa CCM Kirumba huku
wachezaji wake wote wakiwa na ari na morali ya juu tayari kwa kuwakabili the
Flames.
Taifa Stars iliyo chini
ya kocha mkuu Mart Nooij iliwasili jijini Mwanza siku ya jumanne na kufikia
katika hoteli ya La Kairo iliyopo eneo la Kirumba,
ikiwa na kikosi
kamili kwa ajili ya mchezo huo wa kirafiki wa Kimataifa uliopo kwenye
kalenda ya FIFA.
Maandalizi ya mchezo kwa
upande wa Taifa Stars yamekamilika, timu imekua ikifanya mazoezi katika uwanja
wa CCM Kirumba ambao ndio uwanja utakaotumika kwa mchezo.
Wachezaji waliopo jijini
Mwanza ni , Aishi Manula, Mwadini Ali, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Aggrey
Morris, Oscar Joshua, Nadir Haroub, Salim Mbonde, Haji Makame, Hassan Isihaka
na Abdi Banda.
Wengine ni Mwinyi
Kazimoto, Haroun Chanongo, Mrisho Ngasa, Salum Abubakar, Amri Kiemba, Frank
Domayo, Said Ndemla, John Bocco, Juma Luizio, Thomas Ulimwengu na Mbwana
Samatta.
MALAWI YAWASILI MWANZA
Timu ya Taifa ya Malawi
(The Flames) tayari imewasili leo jijini Mwanza majira ya saa sita mchana,
ikiwa na kikosi chake kamili kwa ajili ya mchezo dhidi ya Taifa Stars siku ya
jumapili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.
Malawi imewasili ikiwa
na kikosi chake kamili cha wachezaji 18 na kufikia katika hotel ya JB
Belimonte, wakiwemo wachezaji saba wanaocheza soka la kulipwa katika nchi za
Afrika Kusini, Congo DR, Msumbuji na Zimbabwe.
Wachezaji wa kimataifa
waliowasili ni nahodha Joseph Kamwendo (TP Mazembe -Congo DR), Chimango Kayira
(Costal de Soul - Msumbiji), Frank Banda (HBC Songo - Msumbiji), Esau Kanyenda
(Polokwane City - Afrika Kusini), Harry Nyirenda (Black Leopards - Afrika
Kusini), Limbikani Mzava (Celtic - Afrika Kusini) Gerald Phiri (Caps United -
Zimbambwe)
Wegine ni McDonald
Harawa (Hoyale FC), Richard Chipuwa (Wanderers), Lucky Malata (Silver), John
Lanjesi (Civo), Francis Mulimbika (Wanderers), John Banda (Blue Eagle), Earnest
Tambwe (Surestream) , Micium Mhone (Blue Eagle), Chikoti Chiriwa (Red Lions),
Peter Wadabwa (Silver) na Amos Khamula(Support Ballaton).
Mkuu wa msafara ni
Alexander Waya, Kocha mkuu Young Chimodzi, kocha msaidizi Jack Chamangwana,
kocha wa makipa Pillip Nyasulu, Daktari wa timu Levison Mwale, Meneja wa timu
Frank Ndawa na Afisa Habari James Sangala.
Kikosi cha timu ya Taifa
ya Malawi kinatarajiwa kufanya mazoezi leo saa 10 jioni katika uwanja wa CCM
Kirumba, huku siku ya jumamosi wakipata nafasi ya kufanya mazoezi tena kwenye
uwanja huo wa mchezo.
Kesho jumamosi saa 5 kamili
asubuhi kutafanyika mkutano na waandishi wa habari katika hoteli ya La Kairo
iliyopo Kirumba jijini Mwanza, kocha wa Stars Mart Nooij na kocha wa The Flames
Young Chimodzi wataongelea maandilizi ya mchezo wao wa siku ya jumapili.
0 comments:
Post a Comment