Baada ya kupoteza mchezo wa fainali dhidi ya Barcelona
hapo jana, kipa wa klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Italia Gianluigi ‘Gigi’
Buffon amesema kuwa ataendelea kudaka mpaka atakapofikisha umri wa miaka 40.
Kwa sasa Buffon ana miaka 37 na bado anaamini ana nguvu
za kuweza kudaka kwa miaka mitatu ijayo.
Endapo Buffon atadaka mpaka umri wa miaka 40, atafikia
rekodi ya makipa wengine ambao walifikisha umri huo huku wakidakia vilabu vyao
na timu ya taifa ya Italia.
Makipa hao ni pamoja na Dino Zoff aliyedakia Italia
katika fainali za kombe la dunia la mwaka 1982 akiwa na umri wa miaka 40.
Mbali na Dino zoff, kipa mwingine aliyeweka rekodi ya
kudaka akiwa na umri mkubwa nchini Italia ni Walter Zenga.
Zenga alidakia Inter Milan akiwa na umri wa miaka 39.
Historia inatuonesha kuwa wapo makipa wengi waliowahi
kudaka wakiwa na umri mkubwa katika medani ya soka.
Makipa hao ni pamoja na Brad Fridel wa Marekani amedaka
mpaka akiwa na umri wa miaka 44, Edwin Van Der Sar aliidakia manchester United
mpaka akiwa na umri wa miaka 38.
0 comments:
Post a Comment