Fainali ya pili ya Ligi ya mpira wa kikapu ya NBA
itaendelea tena alfajiri ya kesho kwa kuzikutanisha timu ya Golden State
Warriors na Cleveland Cavaliers.
Katika mchezo wa kwanza timu ya Golden State Warriors
ilipata ushindi wa pointi 108 dhidi ya 100 za Cleveland Cavaliers.
Katika mchezo wa kwanza, Cleveland walimpoteza mchezaji
wao Kyle Irving aliyeumia kifundo cha
mguu na kufanyiwa operesheni ya kifundo hicho huku Kevin Love akiumia bega.
Katika mchezo wa kwanza Lebron James alifunga pointi 44
peke yake na anategemewa sana kufanya vizuri katika mchezo wa leo.
Kwa upande wa Golden State Warriors wenyewe wataendelea
kuwa na wachezaji wake wote nyota ambao ni Stephen Curry, Klay Thompson na
Draymond Green.
0 comments:
Post a Comment