kituo cha Redio Ebony cha mkoani iringa kimepata tuzo kwa upande wa vyombo vya habari kutokana na ushiriki wake kwenye maonesho ya wakulima nane nane kanda ya nyanda za juu kusini yaliyofanyika jijini Mbeya katika viwanja vya John Mwakangale na kuvipiga mweleka vituo vingine vya redio vilivyoshiriki maonesho hayo.
Nafasi ya pili imekwenda kwa televisheni ya taifa TBC na nafasi ya tatu imekwenda Bomba Mm ya jijini mbeya.
Kutokana na tuzo hiyo mtandao huu unapenda kuchukua nafasi ya kutoa pongezi kwa kituo hicho kutokana na jitihada zake za kuwahabarisha watanzania.
Kwa kufuatilia matangazo yake wapate kupitia www.ebonyfm.com au kupitia tune in kama haupo mikoa ya nyanda za juu kusini inapopatikana kupitia masafa ya fm.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment