Timu
ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inaendelea na maandalizi ya mchezo wa kirafiki wa Kimataifa siku ya jumapili dhidi ya
timu ya Taifa ya Malawi (The Flames), mechi itakayochezwa kwenye dimba la
Uwanja wa CCM Kirumba.
Kiugo
mshambuliaji Mwinyi Kazimoto anayecheza soka la kulipwa nchini Qatar
akitarajiwa kuungana na wenzake leo mchana jijini Mwanza.
Mchezaji
Mcha Khamis wa Azam FC amejiondoa kikosini kutokana na kuwa majeruhi, huku
wachezaji wa Young Africans wakitarajiwa kujiunga na kikosi hicho cha timu ya
Taifa mara tu baada ya mchezo wao wa Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya JKT Ruvu siku
ya kesho.
Wakati huo huo Msafara wa watu 25 wa timu ya Taifa ya
Malawi (The Flames) unatarajiwa kuwasili jijini Dar es salaam siku ya alhamis,
kabla ya kuunganisha ndege siku ya ijumaa kuelekea jijini Mwanza.
Katika
msafara huo utakaokuwa na wachezaji 18 na viongozi 7, kocha mkuu wa The Flames
Young Chimodzi amewajumuisha wachezaji nane (8) katika kikosi chake wanaocheza
soka la kulipwa katika nchi za Afrika Kusini, Congo DR, Msumbuji na Zimbabwe.
Wachezaji
wanaocheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini ni Limbikani Mzava (Celtic),
Harry Nyirenda (Black Leopards), Esau Kanyenda (Polokwane City), na Atusaye
Nyondo (University of Pretoria).
Wengine
ni Nahodha Joseph Kamwendo (Tp Mazembe - Congo DR), Frank Banda (HBC Songo -
Msumbuji), Chimango Kayira (Costal De Sol - Msumbuji) na Gerald Phiri (Caps
United - Zimbambwe).
0 comments:
Post a Comment