Mshambuliaji wa kimataifa wa Mexico
Javier Hernandez amekamilisha uhamisho wake wa mkopo kwenda Real Madrid
pamoja na uwezekano wa kununuliwa moja kwa moja kutoka Manchester
United baadaye.
Real inamchukua mchezaji huyo baada ya kufaulu vipimo vya afya leo mjini Madrid.
United inataka
dau la Pauni Milioni 17 kumuuza moja kwa moja mchezaji huyo, lakini kwa
mkataba wa sasa wa mkopo wa muda mrefu wa msimu, Louis van Gaal
anachukua Pauni Milioni 1.5.
United imethibitisha katika ukurasa wake wa Twitter leo kumtoa kwa mkopo mchezaji huyo kwenda Real Madrid.
0 comments:
Post a Comment